Kocha Mkuu wa timu ya Liverpool, Brendan Rodgers amethibitisha kuwa Steven Gerrard amepewa ofa ya mkataba mpya na timu hiyo ya majogoo wa jiji la Merseyside.


Steven Gerrard

Steven Gerrard
Kocha Rodgers amethibitisha kuwa Steven Gerrard (34) atapewa chochote atakacho kihitaji akiwa na timu ya liverpool kwa kuwa alichokifanya kwa miaka takribani (16) ni mchango mkubwa sana na hakuna anayeweza kuilipa fadhila hiyo zaidi ya kumheshimu sana.

 Ikumbukwe pia Gerrard alianzia benchi kwenye mechi yao dhidi ya Stoke city jumamosi ambayo walishinda 1- 0 na ikiwa ni siku yake aliyofikisha miaka kumi na sita (16) tangu alipojiunga na klabu hiyo ya majogoo wa jiji. Pia Brendan alithibitisha kuwa jumapili walikua na mazungumzo na Steven lakini hawakuweza kuwa na maelewano mazuri na kusema kuwa kama akiambiwa amuelezee Captain huyo wa Liverpool basi atakua na maneno mawili tu ya kumuelezea ambayo ni ukweli na heshima kwake kufanya kazi naye na amekuwa akifurahishwa kila dakika aliyofanya kazi na Gerrard na hategemei kumpoteza siku za karibuni.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment