Carragher asema kosa kubwa alilolifanya Wenger katika maisha yake ya soka ni kutomsajili huyu fundi.
-Mchambuzi wa masuala ya soka Jamie Carragher amesema katika maisha ya soka kila mtu amefanya au atafanya kosa ambalo atalikumbuka maisha yake yote, ila akalitaja kosa ambalo kocha wa Arsenal Arsena Wenger alilifanya huko nyuma ambalo mpaka leo linamletea shida, Carragher anasema kama Wenger angemsajili Luis Suarez, mpaka sasa ungekuta Arsenal wameshatwaa kombe la ligi mara mbili au zaidi, mwaka 2013 Arsenal walijaribu kumsajili Luis Suarez kwa kiasi cha paundi milioni 41 lakini Liverpool walikataa na Arsenal wakaachana na dili hilo. Kwa sasa Luis Suarez anafurahia maisha katika klabu ya Barcelona akiwa ameshatwaa kila aina ya kombe huku Arsenal wakiendelea kutaabika kwa kutokuwa na mshambuliaji wa kiwango cha dunia.
0 comments:
Post a Comment