 |
Mourinho akisalimiana na Pochettino. |
Taarifa zinaeleza kuwa mashabiki wengi wa klabu ya Manchester United waliopiga kura kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ujio wa kocha Jose Mourinho katika klabu yao msimu ujao hawajafurahishwa na ujio huo na wengi wao ni waingereza. Jose Mourinho anatarajiwa kuchukua mikoba ya kocha wa sasa Louis Van Gaal mwisho wa msimu atakapokuwa akiachana na klabu hiyo. Mourinho anatarajiwa kupokea dau nono la paundi milioni kumi na tano (15) kwa mwaka. Taarifa za mashabiki hao zinajihirisha kuwa ni kweli Mourinho hapendwi na wengi hasa baada ya juzi kocha wa zamani wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson alipompa nafasi hiyo kocha wa klabu ya Totenham Hotspur Maurcio Pochettino.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment