 |
Ronaldinho akisalimiana na Papa Francis. |
Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya FC Barcelona na mchezaji bora wa dunia mara mbili mfululizo Ronaldinho Gaucho pia ni mshindi wa kombe la dunia mwaka 2002 amefanikiwa kukutana na kiongozi mkubwa duniani wa dini ya Roman Catholic anayetambulika kwa jina la Papa Francis. Ronaldinho alikutana na Papa Francis jana katika jiji la Vatican ambako ndiko yalipo makao makuu ya kanisa Katoliki duniani. Wawili hao walikutana katika shughuli ya kituo cha kutoa elimu kwa vijana kilichozinduliwa na kiongozi huyo wa kidini na walifanikiwa kusalimiana na kuongea mawili matatu kwa muda waliokuwa wamesimama pamoja. Papa anafahamika kwa kupenda sana mchezo wa soka na amewahi kukutana na timu kadha kama Bayern Munich na Juventus pia Papa ni mshabiki mkubwa wa klabu ya nchini kwake Argentina inayoitwa San Lorenzo.
 |
Ronaldinho wakifurahi pamoja na Papa Francis.
|
 |
Ronaldinho wakiagana na Papa. |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment