Barca wavunja rekodi ya Real Madrid.
-Klabu ya FC Barcelona jana ilifanikiwa kuvunja rekodi ya kucheza mechi nyingi bila kufungwa iliyokuwa ikishikiliwa na Real Madrid. Barcelona jana walikuwa wakipambana na Rayo Vallecano kwenye mechi ya La liga na walifanikiwa kuicharaza mabao matano kwa moja huku nyota wa dunia Lionel Messi akipiga hat trick na Ivan Rakitic na Arda Turan wakimalizia shughuli hiyo. Ushindi walioupata Barcelona unawafanya kuwa timu pekee ambayo haijafungwa katika michezo 35 mfululizo na unawafanya kuweka rekodi nyingine Hispania.
0 comments:
Post a Comment