![]() |
Messi akishangilia na Munir El Haddad. |
Katika mechi ya La liga iliyopigwa jana kati ya Eibar na Barcelona iliishia kwa klabu ya Eibar kupokea kichapo kikali cha mabao manne kwa bila (0-4) kutoka kwa FC Barcelona. Eibar waliokuwa nyumbani walishindwa kabisa kufurukuta mbele ya miamba hiyo ya ulaya na dunia. Messi aliiongoza safu ya Barca vizuri kwa kupiga mabao mawili na mwezake Suarez kupiga bao moja huku kinda wa klabu hiyo Munir El Haddad akipiga bao moja katika dakika ya 8 ya mchezo. Mabao mawili ya Messi yanamfanya kufikisha jumla ya mabao 21 katika mechi 23 za la liga alizocheza msimu huu, kwa upande wa Luis Suarez bao lake moja linamfanya kufikisha jumla ya mabao 26 katika mechi 27 alizocheza za la liga msimu huu.
0 comments:
Post a Comment