Wenger; Waacheni waongee nyie pigeni soka.

Arsen Wenger.
Kocha wa klabu ya Arsenal Arsen Wenger akiongea na waandishi wa habari leo amewaambia kuwa yeye ameshazoea watu wanaomponda na hana muda nao zaidi ni kwamba yeye anafuata mambo yake zaidi, Pia Wenger amewataka wachezaji wake kutosikiliza tuhuma hizo na waendelee kupambania ubingwa maana wao hawachezi ili wasishuke daraja bali wanacheza kwa ajili ya ubingwa. Wenger ametuhumiwa kwa kutokuonyesha kiwango bora na wachambuzi wengi wa soka duniani wengine wakiwa ni wachezaji wake aliowahi kuwafundisha, tuhuma hizo zimekuwa nyingi kufuatia kipigo alichokipata juzi dhidi ya Manchester United. Arsenal wanatarajiwa kuikaribisha timu ya Swansea City kwenye mechi ya ligi hapo kesho.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment