 |
Cristiano Ronaldo. |
Taarifa za ndani ya klabu ya Real Madrid zinasema kuwa upo mpango unaosukwa ili kumuuza nyota wa klabu hiyo kwa timu yoyote itakayokuwa tayari kulipa kiasi cha paundi milioni 60. Cristiano Ronaldo anakimbilia kuwa na miaka takribani 32 na tathmini zinaonyesha kuwa ameanza kuchoka kutokana na umri kumtupa mkono, hiyo ni moja ya vitu ambavyo sasa vimeanza kuwashtua mabosi wa Real Madrid na kuwafanya kushusha bei ya mshambuliaji huyo hatari duniani hadi kufikia paundi milioni 60. Klabu za PSG na Manchester United zimekuwa zikitajwa kuwania saini ya mchezaji huyo bora duniani.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment