Kiungo bora kinda wa ligi ya Uingereza asema kuliko aende Arsenal bora astaafu soka.
-Moja ya jambo la kushangaza ni kinda anayefanya vizuri kwa sasa katika ligi kuu ya Uingereza kukataa kujiunga na klabu ya Arsenal (inayofahamika kwa kupenda vijana) kama itatokea siku moja na badala yake atastaafu soka lake. Huyo si mwingine ni kiungo anayekipiga katika klabu ya Totenham Hotspur ya London Dele Alli. Alli alikuwa akihojiwa na waandishi wa habari wakati akiulizwa anajisikiaje kuchaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora mdogo wa msimu na ndipo mwandishi alipomuuliza Je, utapenda siku moja kucheza Arsenal na majibu ya Alli yalikuwa hapana na kuliko nifanye hivyo ni bora nistaafu soka. Dele Alli amefunga mabao nane na kutengeneza mengine tisa kwenye mechi 31 za Epl msimu huu.
0 comments:
Post a Comment