Ozil asema tujilaumu wenyewe.

Mesut Ozil.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil ametoa ya moyoni kuhusiana na mwenendo wa klabu hiyo na kusema kuwa kama wanataka kushinda kitu msimu ujao ni lazima Arsenal wajenge kikosi chenye nguvu ya kupambana na timu zote bila kujali ukubwa au udogo wa timu zinazoshiriki ligi mbalimbali. Ozil alikuwa akihojiwa kwenye mtandao wa "Spox" kuhusiana na Arsenal kupoteza mwelekeo kwenye mbio za ubingwa, ndipo alisema ni kweli tumejimaliza wenyewe na hakuna wa kumlaumu, hatukupaswa kuwa kwenye nafasi tuliyopo kwa sasa lakini bado hatujakata tamaa tutapambana mpaka mwisho. Arsenal wameachwa na viongozi wa ligi hiyo Leicester City kwa tofauti ya pointi 11 huku Arsenal wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment