 |
Nicola Rizzoli. |
Imefahamika kuwa Nicola Rizzoli ndiye refa bora kwa sasa duniani na ndio maana alipewa ridhaa ya kuchezesha mtanange mkali wa jana kati ya Atletico Madrid na Barcelona. Rizzoli jana aliidhihirishia dunia kuwa yeye ndiye refa bora kwa sasa duniani baada ya kuumudu mchezo ambao ulikua na matukio mengi ya kutatiza lakini yeye hakutatizika, moja ya tukio lililoleta kelele nyingi ni lile la kepteni wa Atletico Madrid Gabi kuunawa mpira kwenye eneo la penati lakini Rizzoli aliutoa mpira nje ya box na kuamuru upigwe kama free kick, Maamuzi hayo yamechambuliwa na wadau wengi wa soka duniani na wengi wameona alichokifanya ni sawa maana aliyeupiga mpira ule ni Andress Iniesta ambaye kwa muda huo tayari alipaswa kuwa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kosa la kuunawa mpira makusudi ambapo alisababisha penati lakini Rzzoli hakumuonyesha kadi nyekundu na badala yake alimuonyesha kadi ya njano. Nicola Rizzoli ndiye anayepewa nafasi kubwa kuchezesha mchezo wa fainali ya UEFA utakaopigwa mjini Milano hapo mwezi wa tano.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment