Madrid na Arsenal zashika usukani kwa pesa Ulaya.

Estadio Santiago Bernabeu.
Vilabu vya Real Madrid na Arsenal vimetajwa kuwa ndio wanaoongoza kwa kuwa na utajiri mkubwa na mapato kwa mechi. Klabu ya Real Madrid imetajwa na kampuni ya Deloitte Football Money League kwa mara ya kumi na moja (11) mfululizo kuwa ndio klabu tajiri zaidi ulimwenguni ikiingiza kiasi cha Euro milioni 577 huku ikifuatiwa na Barcelona, Manchester United, PSG, Bayern Munich, Man City na Arsenal ikishika nafasi ya saba huku Chelsea ikishika nafasi ya 8 na Liverpool ikiwa ya 9.
Emirates Stadium.
Kwa upande mwingine klabu ya Arsenal imeweza kuwa ndio klabu pekee barani ulaya inayoingiza mapato makubwa zaidi kwa mechi moja, mapato hayo yanakadiriwa kuwa zaidi ya Paundi milioni mia moja (100) kwa mechi moja, Real Madrid imeshika nafasi ya pili ikiwa inaingiza kiasi cha Paundi milioni 100.12 na nafasi ya tatu imeshikwa na FC Barcelona ikiwa inaingiza paundi milioni 90.17 kwa mechi na nafasi ya tatu na nne zimeshikwa na Manchester United paundi milioni (87.96) na Chelsea paundi (71.84m).
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment