 |
Alexandre Pato. |
Inasadikika kuwa usajili wa aliyekuwa staa wa klabu ya AC Milan na timu ya taifa ya Brazil na sasa Corinthians,
Alexandra Pato umekaribia na mwisho. Mapema leo makubaliano ya awali yamemalizika baina ya Pato mwenyewe na klabu ya Chelsea na kinachosubiriwa kwa sasa ni saini ya Pato tu na si kingine.Wakala wa Pato amekuwa katika mazungumzo ya muda mrefu na mwakilishi wa mmiliki wa klabu ya Chelsea aitwaye
Bi Marina Granovskaia. Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya AC Milan anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka 3 ambao utamwingizia kiasi cha paundi milioni 9. Pamoja na uoga uliopo kwa Chelsea kwamba huenda Pato asiwe fiti kwa sababu hajaichezea Corinthians mechi nyingi, Wakala wake amesisitiza kuwa Pato yuko fiti na ameichezea mara 61 klabu ya Sao Paulo ambayo yuko kwa mkopo.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment