Barca wazidi kumshambulia Cristiano.

Cristiano Ronaldo.
Baada ya mechi ya Jumamosi dhidi ya Atletico Madrid kuisha kwa Real Madrid kupigwa bao moja kwa bila, mshambuliaji wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo alisema kuwa kama kila mchezaji wa klabu hiyo angekuwa kwenye ubora kama wake basi wangekuwa wanaongoza ligi, Kauli hiyo imewapa watu wengi hasira hasa wale mahasimu wa Cristiano na Real Madrid kwa ujumla, Jana Makamu wa Rais wa Barcelona Jordi Mester alisema kamwe hakuna mchezaji wa Barcelona anaweza kutoa kauli kama hiyo maana kabla hawajasajili wachezaji huwa wanaangalia vitu vingi kama tabia n.k. Cristiano Ronaldo amekanusha maana ya kauli aliyoitoa kuwa alikuwa akimaanisha kuwa kila mchezaji angekuwa hana majeruhi kama yeye na si vinginevyo.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment