 |
Cristiano Ronaldo akiwa na rafiki yake kipenzi Badr Hari nchini Morocco mapema wiki hii. |
Taarifa kutoka chanzo kimoja cha habari zinatuarifu kuwa mchezaji nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amekaidi amri ya rais wa klabu hiyo Florentino Perez. Perez alimtaka Ronaldo kuacha mara moja tabia yake ya kwenda nchini Morocco kila mara ili kuonana na rafiki yake mcheza ngumi aitwaye Badr Hari kwa sababu Perez anaamini safari hizo ni moja ya vitu vinavyo hatarisha kiwango cha mchezaji huyo. Pamoja na katazo hilo la Perez bado Cristiano Ronaldo hajaweza kumsikiliza kiongozi wake, baada ya kufunga mabao matatu dhidi ya Espanyol Ronaldo aliamua kutumia muda wa mapumziko wa siku moja kusafiri mpaka Marakhesh Morocco kuonana na rafiki yake huyo. Tukio hilo linaweza kufanya uhusiano wa Perez na Cristiano kuwa hatarini kwa kuwa Perez huwa hapendi dharau hata kidogo na jambo hilo linaweza kuweka hatma ya soka la Ronaldo hatarini.
According to The Huffington Post
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment