Lionel Messi. |
Askari polisi mmoja mwenye umri wa miaka 26 aliyefahamika kwa jina la JM alijitahidi kupiga picha na mchezaji bora wa dunia kipindi kifupi alichokua Dubai lakini hakufanikiwa kwa kuwa Messi alimwambia amechoka kwa kuwa alikuwa amesafiri umbali mrefu, lakini polisi huyo hakuridhika na aliendaa mbali zaidi na kufanikiwa kupata passport ya mchezaji huyo kwenye dawati linalohusika na passport za wasafiri na ndipo alipoichukua passport hiyo na kuchukua video fupi akiwa ameishikilia. Kitendo hicho kimempelekea askari huyo kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha jela kwa muda wa mwezi mmoja.
HAYA NI MANENO ALIYOKUWA AKIYASEMA ASKARI HUYO KWA LUGHA YA KIINGEREZA
“This is Messi’s, he is here in Dubai, what do I do? Shall I burn the passport or just put it back? Ok, ok you can go!”
0 comments:
Post a Comment