Diego costa avunjika pua huku Zuma akiikosa Euro.

Diego Costa.
Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Guus Hiddink ametoa taarifa kuhusiana na mshambuliaji wake hatari Diego Costa. Hiddink akiongea na waandishi wa habari alisema Diego Costa amevunjika pua wakati wa mazoezi ya Alhamisi wakijiandaa kuikaribisha Newcastle kesho. Pia kocha huyo wa Blues amesema kuwa Costa atakuwa uwanjani kupambana na Newcastle huku akiwa amevaa mask, kocha huyo anasema sasa tumekuwa ni timu ya wavaaji maski maana ni wachezaji wengi wanaovaa mask katika timu yetu.
Kurt Zuma alivyoumia kwenye mechi dhidi ya Manchester United.
Taarifa nyingine zinamhusu beki wa kati wa klabu hiyo Kurt Zuma aliyeumia kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya Manchester United. Taarifa zinaeleza kuwa Zuma atakuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungua miezi sita. Taarifa hiyo inamaanisha kuwa Zuma hataweza kucheza michuano ya Euro itakayopigwa nchini kwao Ufaransa. Zuma atafanyiwa upasuaji na daktari Ramon Cugat Jumatano jijini Barcelona nchini Hispania.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment