 |
Louis Van Gaal. |
Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United mholanzi Louis Van Gaal akiongea na waandishi wa habari kuelekea kwenye mechi yao ya leo dhidi ya klabu ya Sunderland amesisitiza kuwa mashabiki wa klabu hiyo wasiwe na wasiwasi kwa kuwa klabu hiyo itamaliza ndani ya timu nne bora za msimu na wataweza kucheza klabu bingwa barani ulaya hapo mwezi wa nane. Manchester United ipo nafasi ya tano ikiwa imeachwa pointi sita na Manchester City inayoshika nafasi ya nne, pia Van Gaal amesema wameshazoea presha na wako tayari kuipambania nafasi hiyo maana uwezo wanao.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment