 |
Manuel Pellegrini. |
Kocha mkuu wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini anajiandaa kucheza kamari kwa kumtumia kepteni wa timu hiyo aliyekuwa majeruhi kwenye mechi ngumu ya kesho dhidi ya Totenham Hotspur. Pellegrini amesema atamtumia Vincent Company kwenye mechi ya kesho dhidi ya Spurs kwa kuwa haoni kama ana shida yoyote, Company alikuwa nje kwa muda wa takribani wiki saba sasa, na matatizo yake ya goti hayapaswi kufanyiwa mchezo kabisa na kama atapata majeraha kwenye mguu huo basi hataweza kucheza tena msimu huu labda msimu ujao. Company ameanza kwenye mechi tatu tu msimu huu na amekuwa nchini Marekani na Ulaya kwa muda akiwa anatibiwa majeraha hayo.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment