Man City waingia vitani na Man United kwa mshambuliaji wa Southampton.

Saido Mane.
Klabu ya Manchester City imeingia katika mbio za kuinasa saini ya mshambuliaji hatari wa klabu ya Southampton na timu ya taifa ya Senegal, Saido Mane. Mane amekuwa akifukuziwa kwa karibu sana na klabu ya Manchester United bila mafanikio, pia imegundulika kuwa Mane hana unusiano mzuri sana na kocha mkuu wa klabu hiyo bwana Ronald Koeman kwa kuwa na utovu wa nidhamu. Gazeti maarufu la "THE SUN" leo limeripoti kuwa Manchester City ipo tayari kumnunua mshambuliaji huyo na ipo tayari kumpa mshahara wake wa paundi laki moja na ishirini na tano (125,000) kwa wiki. Taarifa hizo ni taarifa mbaya sana kwa uongozi wa klabu ya Manchester United.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment