Mashabiki waijia juu Liverpool.

Mashabiki wa Liverpool wakipinga bei za ticket msimu ujao.
Mashabiki wa timu ya Liverpool maarufu kwa jina la majogoo wa jiji wameujia juu uongozi wa timu yao kwa kupandisha bei za viingilio vya msimu ujao kutokana na upanuzi uliofanyika katika uwanja huo. Mashabiki hao wanalalamika kuwa wamepandishiwa viingillio kwa kiasi kikubwa kwani kipindi cha nyuma haikuwahi kutokea mabadiliko makubwa kiasi hicho. Kiingilio cha viti vya bei ya chini kabisa msimu ujao pale Anfield itakuwa ni paundi 36 sawasawa na zaidi ya shilingi elfu 97,200 za kitanzania. "Embu fikiria pesa yote hiyo halafu fikiria jinsi hicho kiti kitakavyo kuwa kibaya" hayo ni maneno ya shabiki mmoja wa Liverpool alipokuwa akielezea hasira zake juu ya bei mpya za ticket. Pia mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakiweka mabango uwanjani yanayosema sisi ni mashabiki wa timu na sio wateja ili kuhimiza uongozi kuwapunguzia bei.

Wamiliki wa klabu ya liverpool, John W Henry na Tom Werner.

Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment