 |
Manchester City. |
Mtandao wa Football Manager 2016 umetoa utabiri wake wa nani atachukua ubingwa wa ligi kuu ya uingereza na nani atacheza Uefa, Europa na watakaoshuka daraja pia. Mtandao huo umeipa klabu ya Manchester City ubingwa kwa msimu huu wa 2016 kwa kumaliza na pointi 80 huku Arsenal ikimaliza na 79 , Leicester City ikimaliza na pointi 69 na Totenham Hotspur wakimaliza na pointi 67 kitu ambacho kitawafanya waweze kushiriki kwenye ligi ya mabingwa.
 |
Jamie Vardy. |
Timu tatu kubwa ambazo kwa siku za hivi usoni na haswa kwanzia msimu umeanza hawajaweza kufanya vizuri, wenyewe wamepewa nafasi ya tano mpaka ya saba, yaani Manchester United watamaliza ligi wakiwa na pointi 66 lakini wakiwa wamefungana pointi pamoja na vigogo wengine wawili yaani Chelsea na Liverpool ila wakiwa na tofauti ya magoli ambapo nafasi ya tano itakuwa imeshikiliwa na Manchester United, nafasi ya sita ni Chelsea na ya saba ni Liverpool.
 |
Msimamo utakavyokuwa mwisho wa msimu according to Football Manager 2016. |
Pia timu iliyopanda ligi msimu huu Bournemouth imetabiriwa kushuka daraja sambamba na Sunderland na Aston Villa. Bila kusahau timu zitakazopanda daraja ni Hull city na Middlesbrough huku Burnley, Derby, Brighton na Cardif wakienda kupambana kwenye mtoano kujua nani atapanda kwenye ligi.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment