 |
Gareth Bale. |
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Gareth Bale akiongea na waandishi wa habari jana, ametoa onyo kwa mahasimu wao FC Barcelona kuelekea mechi yao ya watani wa jadi maarufu kwa jina la "El Classico". Bale amesema japokuwa wapo nyuma kwa pointi kumi bado haiwafanyi kuwa timu iliyokata tamaa kwenye ubingwa wa la liga na kitu cha msingi kwa sasa ni ushindi dhidi ya Barcelona Jumamosi ili waweze kupunguza pengo la pointi mpaka saba. Bale amesema anafurahi sana kucheza chini ya kocha Zinedine Zidane na kila mtu ndani ya klabu hiyo anafurahia uwepo wa kocha huyo na kocha huyo ni moja ya chachu ya upambanaji wa wachezaji walionao. Real Madrid watakaribishwa na FC Barcelona tarehe mbili kwenye uwanja wa Nou Camp kwa ajili ya mechi ya El Classico.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment