Bayern waweka rekodi mpya kwenye UEFA.


Klabu ya FC Bayern Munich jana imeweza kuweka rekodi mbili mpya ambazo hata klabu kubwa duniani kama FC Barcelona haijawahi kuweka. Bayern wamekuwa ni timu ya kwanza kuingia kwenye robo fainali ya klabu bingwa ulaya mara kumi na tano (15), rekodi nyingine waliyoiweka ni kwa kufunga mabao yasiyopungua matatu kwenye mechi (7) za nyumbani. Bayern jana walikuwa na kibarua kigumu dhidi ya Juventus kiasi kwamba walihitaji dakika 120 ili kuvuka hatua hiyo, Bayern walifanikiwa kushinda kwa mabao manne kwa mawili (4-2) dhidi ya Juventus, mabao ya Bayern yalifungwa na Thomas Muller, Kingsley Coman, Thiago Alcantara na Robert Lewandowski huku mabao ya Juve yakifungwa na Paul Pogba na Juan Cuadrado.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment