Messi aweka rekodi mpya kwenye Uefa.
-Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi ameweka rekodi mpya kwenye mashindano ya klabu bingwa ya ulaya jana baada ya FC Barcelona kuwaadhibu Arsenal kwa mabao matatu kwa moja. Lionel Messi alifunga bao la mwisho la Barcelona na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye mashindano hayo kuifunga timu moja mabao 9. Messi anakuwa ni mchezaji wa kwanza kuifunga timu moja mabao 9 kwenye UEFA. FC Barcelona wamefanikiwa kuingia kwenye hatua ya robo fainali ya mashindano hayo kwa kuitoa Arsenal kwa jumla ya mabao matano kwa moja.
0 comments:
Post a Comment