 |
Rafael Benitez. |
Ijumaa mchana ilikuwa ni siku nzuri kwa mhispaniola Rafael Benitez baada ya kutangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Newcastle United baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Steve McCLaren kutimuliwa kazi baada ya timu hiyo kufanya vibaya sana kwenye ligi kitu ambacho kinapelekea klabu hiyo kuweza kushuka daraja. Benitez alipotangazwa tu jana hajasubiri chochote na mara moja ameshawaita wachezaji wa klabu hiyo kwa ajili ya mazoezi kuelekea mechi yao dhidi ya Leicester City itakayopigwa Jumatatu. Wachezaji wa Newcastle walikuwa kwenye siku yao ya mapumziko ila Benitez hajajali hilo.
 |
Benitez akiwa na wachezaji wake mazoezini. |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment