Messi atoa ukweli kuhusu uhusiano wake na Ronaldo.


Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi ametoa ukweli kuhusu uhusiano uliopo kati yake na mchezaji mwenzake Cristiano Ronaldo, Messi akiongea na gazeti la Grafico nchini Argentina amesema kuwa uhusiano wake na Cristiano Ronaldo ni uhusiano wa kawaida na huwezi kusema kuwa ni marafiki ila anamheshimu sana Cristiano na hana ugomvi nae wala timu yake. Messi alizidi kusema kuwa kila mmoja wetu anawakilisha timu yake na kundi la mashabiki wake kwaiyo hakuna uhasama baina yetu na kitu kilichopo ni kwamba kila mtu anatekeleza majukumu yake kwa upande wake. Messi na Cristiano wamekuwa wakipokezana tuzo ya Ballon d`or tangu mwaka 2007 na hakuna mchezaji mwingine aliyeweza kuwaingilia katika hilo, Messi ameitwaa tuzo hiyo mara tano (5) huku Ronaldo akiitwaa mara tatu (3).
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment