 |
Zlatan Ibrahimovich. |
Gwiji wa soka Thierry Henry ni moja ya mashabiki wa Arsenal ambao wanaumizwa sana na mwenendo wa klabu hiyo kwa muda mrefu sana, na sasa ameamua kutaja wachezaji wanaopaswa kusajiliwa na klabu yake hiyo ya zamani. Henry alikuwa akihojiwa na mtandao wa Soccer AM na alisikika akisema nasikia Zlatan kasema anataka kuja Arsenal, nadhani itakuwa ni jambo zuri maana Arsenal inahitaji mchezaji wa aina yake ila kuja kwake kutategemea kama tutamaliza kwenye Top Four maana wachezaji kama hawa wanataka kucheza Uefa, Pia Henry alisema Arsenal inamuhitaji kiungo mkabaji wa timu ya Leicester City N`golo Kante. Arsenal leo wanapambana na Watford kwenye kombe la FA.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment