Wenger aponda maneno ya Sanchez.


Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Arsen Wenger akiongea na waandishi wa habari kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Totenham Hotspur amesema kuwa haoni kama kuna ukweli wowote kuhusiana na madai yaliyotolewa na mshambuliaji wa klabu hiyo Alexis Sanchez kuwa timu hiyo haina hari au hasira ya kuchukua ubingwa na pia haijiamini. Wenger akitolea ufafanuzi swala hilo amesema hayo ni maneno ya Sanchez lakini anachokiona yeye ni jambo la kawaida kupoteza mechi na hadhani kama timu yake imepoteza muelekeo katika mbio za ubingwa, Alipoulizwa kuhusu mechi ya kesho dhidi ya Spurs alisema ligi imekuwa haitabiriki kwaiyo chochote kinaweza kutokea. Arsenal kesho itapambana na Totenham Hotspur katika uwanja wa Whitehart Lane majira ya saa 9:45 alasiri.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment