 |
Marcus Rashford. |
Mchezaji bora wa mwezi wa pili wa klabu ya Manchester United amecheza dakika 170 tu mpaka sasa na amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo bila shida. Manchester United imemtangaza kinda wake Marcus Rashford kuwa ndiye mchezaji bora wa klabu hiyo kwa mwezi February na kumfanya kuwashinda wakongwe aliowakuta katika timu ya kwanza (First Eleven). Rashford amecheza mechi tatu tu mpaka sasa na amefanikiwa kufunga jumla ya mabao manne na kutengeneza lingine moja, Rashford alianza kufunga kwenye mechi ya klabu bingwa ulaya (EUROPA) dhidi ya FC Midtjylland na alifanikiwa kufunga jumla ya mabao mawili kwenye ushindi wa 5-1, hakuishia hapo tu mechi iliyofuata aliwaadhibu vibaya Arsenal kwa kuwapiga mabao mawili na kutengeneza moja kwenye ushindi wa mabao 3-2. Rashford pia alicheza mechi dhidi ya Watford na hakufanikiwa kuziona nyavu japokuwa alionyesha soka safi kabisa. Rashford amewashinda wakongwe kadhaa kwenye tuzo hiyo kama Juan Mata aliyecheza dakika (590), Jesse Lingard (595), Ander Herrera (351), David De Gea (360) na Anthony Matial (420).
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment