 |
Antonio Conte. |
Klabu ya Chelsea leo mchana imeamua kumtangaza kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte kuwa ndiye kocha atakayewaongoza msimu ujao. Chelsea imeamua kufikia uamuzi huo baada ya hapo awali kumtimua kocha wao aliyewapa ubingwa msimu uliopita Jose Mourinho baada ya kuboronga karibia nusu msimu. Kocha wa sasa wa klabu ya Chelsea Guus Hiddink ataachia ngazi mwisho wa msimu huu ili kumpisha Conte aweze kuanza kazi na timu hiyo kwenye msimu mpya. Conte anakumbukwa kwa mafanikio aliyoyapata akiwa na klabu ya Juventus. Taarifa za awali zinasema kuwa Conte amesaini mkataba wa miaka mitatu na miamba hiyo ya darajani.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment