Wenger achukizwa na maneno ya Ozil.

Arsen Wenger.
Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Arsen Wenger akiongea na waandishi wa habari jana kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Watford, Wenger amesema kauli kama za Ozil hazikubaliki kwenye klabu hiyo haswa kipindi hiki cha kugombania ubingwa wa England. Ozil alikaririwa na vyombo vya habari katikati ya wiki hii akisema kuwa Arsenal imepoteza Ubingwa kwa uzembe wao wenyewe na hakuna wa kumlaumu, maneno hayo yamemkera sana Wenger kiasi cha kumfanya aseme mbele ya waandishi wa habari kuwa maneno hayo hayakubaliki hata kidogo. Leo Arsenal wapo uwanja wa nyumbani wakiikaribisha klabu ya Watford kwenye mchezo wa ligi.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment