Gabriel; Koscienly ni moja ya mabeki bora wa kati duniani.
-Beki kutoka Brazil Gabriel Paulista amempongeza beki mwenzake wanayecheza naye katika klabu ya Arsenal Laurent Koscienly na kusema kuwa ni moja ya mabeki bora kabisa wa kati duniani hivi sasa. Gabriel amekuwa moja ya wachezaji muhimu sana siku za usoni katika kikosi cha Wenger ambapo amechukua nafasi ya Mjerumani Per Mertersacker ambaye amepigwa benchi kutokana na kupoteza kiwango chake. Wenger amemsifia Gabriel na kumfananisha na Koscienly kitu ambacho kimemfurahisha sana Gabriel kiasi cha kumfanya aseme hayuko mbali sana kufikia kiwango cha beki huyo kisiki kutoka nchini Ufaransa. Koscienly na Gabriel wanatarajiwa kutengeneza ukuta imara wiki end hii watakapomenyana na West Ham.
0 comments:
Post a Comment