Neymar amtaka Pogba Barcelona.
-Mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona Neymar ameamua kuweka hisia zake wazi wazi kuhusiana na jinsi anavyomkubali kiungo wa kifaransa anayechezea klabu ya Juventus Paul Pogba na kuamua kusema kuwa angependa siku moja acheze na kiungo huyo Barcelona. Neymar alipokuwa akihojiwa na mtandao wa Uefa Champions League aliulizwa kuhusu ni nani angependa kupata fulana yake kama kumbukumbu alisema ninazo nyingi ila kwa sasa natamani kupata ya Pogba maana ni mdogo na anavyocheza soka inavutia zaidi. Neymar na Pogba walikutana kwenye fainali iliyopita ya UEFA ambapo Barcelona waliichapa Juventus mabao matatu kwa moja.
0 comments:
Post a Comment