Mamadou Sakho asema mchezaji mwenzake ni bora kuliko Messi na Ronaldo.
-Beki wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa Mamadou Sakho akiongea na mtandao wa Bein Sport amesema amewahi kucheza dhidi ya "Cristiano Ronaldo na hata Messi lakini sijaona kama walikuwa na makali aliyokuwanayo Haterm Ben Arfa, sijui labda hawakuwa kwenye ubora wao ila Ben Arfa ni moto wa kuotea mbali nimewahi kucheza dhidi yake alipokuwa klabu ya Lyon". Ben Arfa aliwahi pia kucheza klabu ya Newcastle kabla ya kurudi kwenye ligi yake ya nyumbani ya Ufaransa na uwezo wake mpaka sasa umemfanya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment