Pellegrini amtaja mchezaji bora wa ligi ya Uingereza kwa msimu huu.
-Kocha wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amesema ni jambo la ajabu na la kushtua inakuwaje mchezaji mzuri na bora kama Sergio Aguero hajawahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu yaani PFA. Pellegrini amesema kwa msimu huu anaona ni bora wampe Aguero maana hakuna mchezaji aliyekaribia ubora wake, Pia Pellegrini ametoa pongezi za dhati kwa wachezaji wake haswa Aguero na De Bruyne kwa kuisaidia klabu hiyo kupata matokeo mazuri dhidi ya Chelsea jana kwenye uwanja wa Stamford Bridge, Aguero alifunga mabao yote matatu.
0 comments:
Post a Comment