Zidane asema Ronaldo ndiye mchezaji bora zaidi duniani kwa sasa.


Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amefunguka na kusema kuwa kwa sasa duniani hakuna mchezaji kama Cristiano Ronaldo, Zidane anasema kuwa Ronaldo anaonyesha yeye ni mtu wa aina gani kwa vitu anavyovifanya na ndivyo vinavyomfanya aonekane kuwa mtu wa tofauti, pamoja na hayo bado anahitaji wachezaji wenzake kumi ili kukamilisha anachokifanya ndiyo maana kila mchezaji ana umuhimu kwenye timu ila sio kila mchezaji anaweza kufunga mabao matatu kwenye mechi moja tena yenye msisimko kama ya leo. Zidane pia ameipongeza timu yake nzima kwa ujumla na akaitaka izidi kushikamana ili kunyanyua la decima ya kumi na moja na kuiletea Real Madrid heshima kubwa duniani kote.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment