Baada ya kuisambaratisha Wolfsburg Cristiano ataja anaowataka nusu fainali.


Mshambuliaji hatari duniani kwa sasa Cristiano Ronaldo jana aliongoza mauaji ya kutisha kwa timu kutoka Ujerumani kwenye mchezo wa robo fainali ya klabu bingwa ya Ulaya. Ronaldo alifanikiwa kuisaidia klabu yake ya Real Madrid kuvuka hatua ya robo fainali na kwenda nusu fainali baada ya kuichapa Wolfsburg mabao matatu kwa sifuri (3-0) kwenye mchezo wa jana, Baada ya mchezo huo Cristiano Ronaldo alihojiwa na baadhi ya waandishi wa habari kuhusiana na namna anavyojisikia na angependa hatua ya nusu fainali wakutane na timu gani, Ronaldo alijibu na kusema kuwa anajisikia faraja sana kuivusha timu yake kwenye hatua hii ngumu na angependa kwenye hatua ya nusu fainali wakutane na Benfica.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment