Pardew awa kocha mpya wa Crystal Palace.

Alan Pardew, kocha mpya wa crystal palace
Klabu ya Crystal Palace hivi punde imemtangaza Alan Pardew (53) kuwa kocha wao mpya kuanzia sasa. Alan Pardew alikuwa kocha wa klabu ya Newcastle United kuanzia mwaka 2010 na aliweza kuipatia mafanikio makubwa tu kabla ya msimu huu kuanza vibaya na mashabiki wa timu hiyo kutaka afukuzwe haraka iwezekanavyo lakini haikuwa rahisi hivyo kwa kuwa kocha huyo alikuwa na mkataba mrefu na timu hiyo kitu ambacho kilimfanya mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kushindwa kumfuta kazi lakini baadaye Pardew aliiwezesha timu hiyo kurudi kwenye fomu nzuri ambapo inakumbukwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa kocha wa kwanza kumfunga Josee Mourinho na kikosi chake cha Chelsea msimu huu kabla ya juzi Mauriccio Pochentino kufanya hivyo tena akiwa na klabu ya Totenham Hotspur.
Alan Pardew, picha ndogo akiwa mchezaji wa crystal palace.
Pia Alan Pardew aliwahi kuichezea timu hiyo ya Crystal Palace hapo mwanzo na ndiyo maana imekuwa rahisi kwake kukubali ofa hiyo ya miaka mitatu na nusu ya kujiunga na klabu yake ya zamani. Alan Pardew ameushukuru uongozi mzima wa Timu ya Newcastle United na timu nzima kwa ujumla kwa kuwa na imani nae kwa kipindi hicho chote.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment