 |
Neymar JR. |
Imefahamika kuwa klabu ya Real Madrid imekuwa ikimfukuzia mshambuliaji hatari wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Neymar da Silva kwa karibu zaidi na hivi majuzi kulizuka taarifa kuwa Neymar na baba yake ambaye ndiye wakala wake walikutana na wawakilishi wa klabu ya Real Madrid kule Zurich Uswiz ambako kulifanyika sherehe za kutoa tuzo za wachezaji bora wa dunia na imefahamika kuwa walizungumza mambo kadhaa kuhusu hatima ya Neymar pale Barcelona baada ya kutakiwa kuongeza mkataba wake na kuanza kulipwa kiasi cha Euro milioni 19. Gazeti maarufu nchini Hispania la michezo liitwalo LA MARCA leo limeripoti kuwa klabu ya Real Madrid ipo tayari kutoa kiasi kikubwa cha euro milioni 190 kilichopo katika mkataba wake wa sasa ili kumng`oa Neymar Barcelona, Pia imefahamika Real Madrid itapaswa kuuza mchezaji wake mmoja Star ili kupata pesa ya kujazilishia euro milioni 190.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment