Barcelona na Madrid zachezea kichapo La liga.
-Klabu bingwa ya dunia na ulaya Real Madrid jana walikua wakitafuta ushindi wa ishirini na tatu mfululizo katika ligi yao ya nyumbani maarufu kama la liga pale katika uwanja wa Mestalla walipokutana na wenyeji Valencia. Real Madid ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya kumi na tatu ambapo Cristiano Ronaldo alikwamisha mpira kimiani kwa njia ya mkwaju wa penalti na kufanikiwa kufikisha bao lake la 26 kwa msimu huu katika ligi na bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza kilipomalizika, Valencia waliporudi kipindi cha pili hawakutaka masihara na katika dakika ya 52` Barragan alifanikiwa kuiandikia timu yake bao la kusawazisha kabla ya Otamedi kuandika bao la ushindi katika dakika ya 65` na kufanya mchezo kuisha kwa Valencia kuichapa Real Madrid (2-1).
Kwingineko huko katika uwanja wa Real Sociedad kulikuwa na mtanange wa kutisha uliozikutanisha klabu za FC Barcelona inayofundishwa na Luiz Enrique na Real Sociedad inayofundishwa na aliyekuwa kocha wa Manchester United na Everton "David Moyes". Barcelona walianza mchezo bila ya wachezaji wao nyota kama Lionel Messi, Dani Alves na Neymar Jr ambao wote walifanikiwa kuingia katika kipindi cha pili lakini bado hawakuisaidia Barcelona kurudisha goli la dakika ya pili ambalo beki Jordi Alba alijifunga na mpaka mchezo unakwisha matokeo yalisomeka Real Sociedad 1-0 FC Barcelona.
0 comments:
Post a Comment