Mahrez aweka rekodi.

Riyad Mahrez.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Leicester City na timu ya taifa ya Algeria Riyad Mahrez ambaye amefunga mabao kumi na saba msimu huu na kuwawezesha Leicester kufuzu kucheza klabu bingwa ya Ulaya msimu ujao amekuwa ndiye mchezaji wa kwanza mwenye asili ya Afrika kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Uingereza (PFA) tangu ianzishwe. Mahrez amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo jana kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Grosveno Hotel jijini London jana usiku. Katika sherehe hizo Dele Alli kiungo wa Spurs alifanikiwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi huku Jamie Vardy akitwaa tuzo ya heshima kwa kuvunja rekodi kibao msimu huu. Ryan Giggs nae alifanikiwa kupata tuzo ya heshima kwa kuitumikia klabu yake kwa ngazi zote za uchezaji na ukocha pia.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment