Podolski akaribia kuikacha Arsenal.

Lukas Podolski akiwa uwanja wa ndege wa Milan.
Mshambuliaji wa Arsenal, Lukas Podolski (29) anakaribia kumaliza sakata lake la kujiunga na kocha Roberto Mancini katika timu ya Inter Milan ya huko Italia. Lukas Podolski amesafiri mpaka mjini Milan kwa ajili ya kumalizia mazungumzo ya mwisho ya kujiunga na miamba hiyo ya italia na amefanikiwa kupata mapokezi ya ajabu kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo katika uwanja wa ndege, Pia inasemekana kwamba atajiunga na miamba hiyo kwa mkopo wa miezi sita kabla ya kufanyika kwa usajili wa moja kwa moja utakaogharimu paundi milioni 5.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment