 |
Gareth Bale |
Winga wa mabingwa wa dunia na ulaya (Real Madrid) Gareth Bale amethibitisha kuwa ana furaha kubwa sana kuwa sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo ikiwa mpaka sasa ameshashinda mataji makubwa kama klabu bingwa ya dunia, klabu bingwa ya ulaya (UEFA), kombe la mfalme (COPA DEL REY) na hana mpango wowote wa kuondoka katika klabu hiyo yenye maskani yake Estadio Santiago Bernabeu na wala hazipi nguvu tetesi za yeye kujiunga na mashetani wekundu (Manchester United).
.jpg) |
Wilfred Bony. |
Kwa upande mwingine huko Ligi ya Uingereza kumekucha kwani mshambuliaji wa Swansea City anawindwa kwa karibu na vigogo wa ligi hiyo ambao ni Chelsea na Man City, huku klabu ya Man City ikionekana kuwa mstari wa mbele kwani kwa sasa hawana straika kutokana na majeruhi ya Sergio Aguero na Edin Dzeko.
 |
William Carvalho |
Na kwingineko huko Ureno habari zilizosambaa ni kwamba washika bunduki wa jiji la London Arsenal wanaongoza katika mbio za kumsaini kijana mdogo wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Ureno "William Carvalho" (25) kwa paundi milioni 25 na ikizingatiwa kwamba Arsenal wamekua na uhitaji mkubwa wa kiungo mkabaji, wadau wa Arsenal wanaomba Mungu kocha wao Arsene Wenger asibadilishe mawazo kama kawaida yake.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment