SANOGO ATIMKIA CRYSTAL PALACE.



Mshambuliaji kinda wa timu ya Arsenal, Yaya Sanogo mwenye miaka (21) na ambaye ameichezea klabu yake hiyo ya London mara sita tu msimu huu, ameamua kutimkia Crystal Palace kwa mkopo kwa kipindi chote cha msimu huu kilichobaki ili kusaka makali kwakua hivi sasa ndani ya timu yake kumekua na ushindani mkubwa wa namba kitu kilichosababisha pia Lukas Podolski kutimkia Inter Milan ya Italia. Yaya Sanogo aliweza kuichezea Arsenal mara kumi na nne msimu uliopita ikiwamo mechi za nje nne na fainali ya kombe la FA, pia Yaya Sanogo ameweza kuifungia timu yake ya taifa ya chini ya miaka (21) magoli matatu katika mechi nne.

Kwa ujumla Yaya Sanogo ni mchezaji mzuri na amekwenda Crystal Palace kupata uzoefu wa kupata namba kikosi cha kwanza
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment