Wilfred Bony atua Man City.
-Mshambuliaji wa klabu ya Swansea na timu ya taifa ya Ivory Coast, Wilfred Bony amejiunga rasmi na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza kwa kiasi cha paundi milioni 28. Wilfred Bony (26) amepatiwa jezi namba 14 na hataweza kuichezea klabu yake hiyo mpya kwa sasa mpaka katikati ya mwezi Februari kutokana na kuwa na majukumu ya timu yake ya taifa huko Equtorial Guine ambako wanacheza mashindano ya kombe la Afrika (AFCON). Man City wametangaza katika akaunti yao ya twitter.
0 comments:
Post a Comment