DEFOE ATUA SUNDERLAND NA NASRI KUIKOSA ARSENAL JPILI.

Jermain Defoe.
Mshambuliaji wa timu ya Toronto Fc, Jermain Defoe (34) amerudi katika ligi ya Uingereza na sasa amesaini mkataba katika klabu ya Sunderland mchana huu kwa dau la paundi milioni 3.2 kwa mwaka mmoja na mechi yake ya kwanza itakua dhidi ya klabu yake ya zamani Totenham Hotspur kama atapata kibali cha kufanya kazi Uingereza kesho saa 8 mchana.

Na kwingineko huko katika jiji la Manchester katika kambi ya Man City, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo na mchezaji wa zamani wa Arsenal, Samir Nasri ataukosa mpambano wa kukata na shoka hapo jumapili katika dimba la Etihad kutokana na maumivu ya misuli aliyoyapata katika mechi iliyopita walipocheza na everton na anategemewa kuwa nje kwa muda wa wiki tatu alieleza kocha wa Man City, Manuel Pellegrin na kusisitiza kuwa Vicent Kompany na Sergio Aguero watakuwa fiti kwa asilimia mia moja 100% kwa ajili ya mpambano huo.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment