Arsenal, Barca na Man City zaua Liverpool yavutwa shati.

Mohamed Elneny.
Arsenal leo imeweza kuwachapa timu ngumu ya Burnley katika mechi ya kombe la FA iliyopigwa katika dimba la Emirates na kushuhudia wenyeji Arsenal wakiibuka na ushindi wa bao mbili kwa moja (2-1), Arsenal ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa beki wake wa kulia Colum Chambers aliyepigiwa pande safi na Alexis Sanchez lakini haikupita mda mrefu kabla Vokes wa Burnley hajaisawazishia timu yake kwa bao safi la kichwa, mpaka mapumziko timu hizo zilikuwa sare na ilipofika kipindi cha pili mnamo dakika ya 58 Alexis Sanchez alipiga bao la pili kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Alex Oxlade Chamberlain, na mpaka mchezo huo unafikia ukingoni mabao yalikuwa ni mbili kwa moja.

Kelechi Iheanacho.
Kwingineko katika mechi nyingine za FA, tumeshuhudia klabu ya Manchester City ikitoa kipigo kikali kwa timu dhaifu ya Aston Villa cha mabao manne kwa bila (0-4) huku mshambuliaji wake kinda Iheanacho akitupia hat-trick na Rahim Sterling akimalizia bao moja. Matokeo mengine ni kama yafuatavyo;

Joe Allen akijaribu kumtoka beki wa West Ham.
1. Colchester 1 - 4 Totenham.
2.Liverpool 0 - 0 West Ham.
3. Crystal Palace 1 - 0 Stoke City.

Luis Suarez.
Huko Hispania kwenye ligi yao maarufu kama La Liga kulikuwa na mechi nyingi tu ila kubwa zaidi ilikuwa baina ya miamba miwili yaani FC Barcelona na Atletico Madrid na kufanikiwa kuisha kwa FC Barcelona kumuadhibu Atletico Madrid kwa jumla ya mabao mawili kwa moja (2-1), Atletico ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 9 kupitia kwa Koke na Messi alifanikiwa kusawazisha dakika ishirini baadae kabla muuaji Luis Suarez hajawamaliza vijana hao wa Diego Simeon katika dakika ya 38 ya mchezo, pia Atletico walimaliza mchezo huo wakiwa tisa baada ya kupigwa kadi nyekundu mbili.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment