 |
Matt Miazga akiwa daktari mkuu wa klabu ya Chelsea, Michael Emenalo. |
Imefahamika kuwa klabu ya Chelsea imefanikiwa kumnasa beki wa klabu ya New York Redbulls mwenye umri wa miaka 20 aitwaye Matt Miazga kwa dau linalodhaniwa kuwa kiasi cha paundi milioni 3.5. Matt Miazga anafahamika kwa kuwa mmoja wa mabeki bora zaidi katika ligi ya Marekani maarufu kama MLS na uhodari wake umemuwezesha kuingia katika kikosi cha taifa kinachonolewa na Jurgen Klinsmann. Beki huyo alikuwa amebakiwa na miezi 12 tu katika mkataba wake kabla hajasaini Chelsea dili la miaka minne na nusu. Chelsea imefanikiwa kuinasa saini ya beki huyo baada ya kuzishinda Leicester City, Manchester City na Stoke City zote zilikuwa zikimfukuzia beki huyo kisiki.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment