 |
Olivier Giroud. |
Mshambuliaji hatari kwa sasa wa klabu ya Arsenal, Olivier Giroud amesema watu wengi wanaomponda kuhusu kiwango chake pale Arsenal hawamnyimi usingizi hata kidogo na safari hii anatarajia kufunga goli zipatazo 30. Giroud amekuwa akilaumiwa na mashabiki wengi wa Arsenal kwa kushindwa kuonyesha kiwango kinachostahili kuonyeshwa na mshambuliaji namba 9, Pia wachezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal kama Thiery Henry wamekuwa wakimweleza Wenger kuwa Giroud hawezi kumpa ubingwa hata siku moja na anahitaji kusajili mshambuliaji mwingine ili aweze kusaidiana na Giroud lakini Wenger amekataa kufanya hivyo na amesema yeye anamuamini Giroud. Takwimu zinaonyesha Olivier Giroud ndiye mchezaji aliyeibeba Arsenal msimu huu kuliko mchezaji mwingine yeyote akiwa amefunga mabao 18 mpaka sasa na 11 yakiwa ya kwenye ligi na mengine kwenye ligi ya mabingwa ulaya na akikumbukwa pia kwa kuiwezesha klabu yake kutinga hatua ya 16 bora kwa kufunga mabao matatu katika mechi dhidi ya Olympiacos.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment